July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Naibu Spika awapongeza wabunge Mwambe, Rose kuoana, awapa darasa

Wabunge Cecil Mwamba na Rose Tweve

Spread the love

 

NAIBU Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu leo tarehe 27 Mei, 2022 amewapongeza wabunge Cecil Mwamba na Rose Tweve wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufunga ndoa hivi karibuni na kuongeza kuwa ni neema kwa Bunge hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala (CCM) ametoa darasa kwa wabunge wanaume kwamba wasio mwanamke mzuri pekee bali waoe mwanamke mwema vivyo hivyo wanawake wasiolewe na mwanamume mzuri pekee bali waolewe na mwanaume mwema.

Zungu ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma baada ya kipindi cha maswali na majibu ambapo pamoja na mambo mengine amesema jana tarehe 26 Mei, 2022 alimuona Rose Tweve (Mbunge Viti Maalumu Iringa) ndani Bunge.

Naibu Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu

“Kwa kweli lazima niwapongeze kwa wabunge wawili kuoana humu ndani ni neema kwetu.

“Sidhani kama na nyie mligundua kuna vitu vinapitapita lakini wamefanya heshima na wamefanya staha mpaka kufikia kuunganisha roho zao pamoja,” amesema na kuongeza;

“Kwa hiyo ninawapongeza sana… usioe mke mzuri, oa mke mwema kwa sababu uzuri unakwisha wema hauishi na usitake kuolewa na mwanaume mzuri, olewa na mwanaume mwema kwa sababu uzuri unakuisha wema hauishi,” amesema.

Amesema jana hakumuona Cecil Mwambe ambaye ni Mbunge wa Ndanda (CCM) na leo wote hawapo hivyo inawezekana wanafuatilia cheti cha ndoa yao.

error: Content is protected !!