February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Naibu Meya wa Dar atimkia CCM

Mussa Kafana, Aliyekuwa Naibu Meya Dar es Salaam

Spread the love

ALIYEKUWA Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mussa Kafana amejiuzulu uanachama wa CUF na kuomba kupokelewa ndani ya CCM. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kafana ambaye pia alikuwa diwani wa kata ya Kiwalani ametangaza kujivua uanachama wa CUF pamoja na kujiuzulu udiwani na unaibu meya wa jiji la Dar es Salaam leo tarehe 18 Agosti, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa.

Akielezea sababu za kujiuzulu, Kafana amesema mgogoro unaoendelea katika chama hicho unamyima fursa ya kisiasa na hivyo amemaua kuhamia katika chama kisicho na migogoro.

“CUF ina pande mbili zinavutana na mngogoro huu hauwezi kuisha leo wala kesho kwa sababu wanachobishana na kuvutana ni watu wakubwa kwenye chama. Sijaongea na kiongozi yoyote wa CCM na sijajiunga na chama chochote cha siasa ila kama viongozi wa chama hicho wananisikia na watanipokea nitashukuru naomba nipokelewe,” amesema Kafana.

error: Content is protected !!