May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Naddy kuwapandisha jukwaani wasanii Dar

Spread the love

MSANII wa muziki wa bongo fleva Nandela Charles Mfinanga maarufu Nandy leo Jumamosi tarehe 4 Septemba 2021 anahitimisha kilele cha tamasha lake ‘Nandy Festival. Anaripoti Matilda Peter… (endelea)

Tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Kigoma tarehe 6 Juni 2021, litahitimishwa katika viwanja vya Posta, Kijitonyama mkoani Dar es Salaam na kuwakutanisha wasanii mbalimbali nchini humo.

Miongoni mwa mikoa aliyopita; ni Mwanza, Arusha, Mtwara, Dodoma na Zanzibar ambako kila alikopita alikonga nyonyo za mashabiki zake akiwa na wasanii kama Alikiba, Lina Sanga, Babalevo, Mr blue, Fid q na Whozu.

https://www.youtube.com/watch?v=YxnxkbO7Kug

Wasanii mbalimbali wa watahitimisha kilele hicho leo Jumapili akiwemo Willy Paul kutokea nchini Kenya.

Kutoka Tanzania, watakaopanda jukwaani; ni Baba levo, Young lunya, Juma Nature, Rosa ree, Linah Sanga, Whozu, Dullah Makabila, Sholomwamba, Weusi, Saraphina, Mabantu na Juma Jux.

error: Content is protected !!