Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu NACTVET yafungua dirisha la udahili
Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love

 

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefungua dirisha la udahili wa mkupuo wa mwezi Machi kwa mwaka wa masomo wa 2023/24 kuanzia tarehe 16 Januari 2023. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo imesema kwamba vyuo vyote vinaruhusiwa kudahili wanafunzi katika mkupuo huu, isipokuwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi kwa Tanzania Bara.

Taarifa hiyo imesema vyuo vya Afya na Sayansi shirikishi vilivyopo Tanzania Visiwani vyenye uwezo wa kudahili katika mkupuo huo vinaruhusiwa ikiwa vitakidhi vigezo.

Katika taarifa yake hiyo, NACTVET limevielekeza vyuo vinavyohitaji kudahili wanafunzi kwa mkupuo huu kutuma maombi yao kabla ya tarehe 27 Januari 2023 kwa kujaza fomu inayoonesha uwezo wa chuo kuendesha mafunzo na kuiwasilisha katika ofisi za Kanda za Baraza ambapo chuo husika kipo.

“Uwezo huo ni pamoja na kuwa na miundombinu na walimu wa kutosha kutoa mafunzo katika mikupuo miwili kwa mwaka (Machi na Septemba)” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Baraza hilo limesema kwamba fomu ya maombi inapatikana katika tovuti ya Baraza hilo www.nacte.go.tz kwa kubofya fomu ya maombi ya udahili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

error: Content is protected !!