July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NACTE yafuta vyuo vitatu

Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Dk. Adolf Rutayuga akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Mitaala wa NACTE, Twilumba Mponzi

Spread the love

KATIKA jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishushia hadhi vyuo 16. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Vyuo hivyo ambavyo vimefutiwa usajili ni Dar es Salaam College of Clinical Medicine kilichokuwa na usajili wa awali, Ndetele School of Medical Laboratory Sciences, na Institute of  Information Teknology vyote vya Dar es Salaam.

Vilivyoshushwa hadhi ni pamoja na Sura Technologies- Dar, Institute of Management and Information Technology- Dar, Techno Brain- Dar, Ministry of Agricukture Training Institute Igurusi- Mbeya, Mbozi School of Nursing -Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School- Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School -Moshi.

Vingine ni Advanced Pediatrics Nursing KCMC Moshi, AMO Training Centre Tanga, CATC Songea, CATC- Sumbawanga, COTC Maswa- Shinyanga, COTC -Musoma, Dentak Therapists Training Centre- Tanga, Ndudu School of Environmenta- Kwimba na KCMC AMO General School Moshi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga amesema kuwa, hatua hizo zimefikiwa baada ya vyuo vingi kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE.

“Kwa kutumia sheria za Bunge  sura Na.129 na kanuni za Baraza za usajili (2001), 20 Februari 2015, baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa Taasisi na vyuo vya umma. Notisi ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho ya makosa yaliyobainishwa,” amesema Rutayuga.

Amesema, kunabaadhi ya vyuo ambavyo vilivyofanyia kazi upungufu wao baada ya notisi kutolewa lakini kuna vingine vilikaidi maagizo hayo, hivyo havikuchukua hatua yoyote.

Aidha, baraza limechukuwa hatua hizo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake ambapo walibaini makosa yafuatayo;-

Kumalizika kwa muda wa usajili wa awali, kutoanza mchakato wa kupata ithibati baada ya kupata usaili kamili, kumalizika kwa muda wa ithibati, kutochukua hatua ya kuomba upya ithibati na vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.

Hata hivyo Rutayuga amesema, wanafunzi ambao wapo katika vyuo vilivyofutiwa usajili watapatiwa ufumbuzi na kupelekwa kwenye vyuo vyenye usajili kupitia NACTE.

Rutayuga ametoa wito kwa wazazi pamoja na wanafunzi kuvichunguza vizuri vyuo kabla ya kujiandikisha ili kuepuka matatizo na uzembe unaofanywa na uongozi wa chuo husika.

error: Content is protected !!