Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Maisha Burudika Nabii mrembo, bilionea Lucy Natasha achumbiwa na Nabii wa Kihindi
Burudika

Nabii mrembo, bilionea Lucy Natasha achumbiwa na Nabii wa Kihindi

Spread the love

 

“Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, nikamuona mpendwa wa nafsi yangu, nikamshika, nisimuache tena, hata nilipomleta nyumbani mwa mama yangu, chumbani mwake aliyenizaa.”

Huo ni ujumbe mwanana wa neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Biblia Takatifu katika Wimbo Ulio Bora 3:4 uliotolewa Mwinjilisti na Nabii wa Kimataifa kutoka nchini Kenya, Lucy Natasha wakati akimtambulisha mchumba wake anayefahamika kwa jina la Stanley Carmel.

Natasha mwenye umri wa miaka 29, ndiye mchungaji mwanzilishi na kiongozi wa kanisa la The Empowerment Christian Church (ECC) lililopo katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Tarehe 27 Novemba mwaka huu alianza kugusia suala la kuchumbiwa na siku iliyofuata Jumapili tarehe 28, alipakia picha za kuvalishwa pete na kumtambulisha rasmi mchumba wake huyo, Stanley Carmel baada ya tukio hilo kufanyika katika kanisa kwake.

Picha hizo aliziweka katika akaunti zake za mitandao yote ya kijamii huku akisindikiza na jumbe kadhaa kutoka katika kitabu cha Biblia.

Wawili hao walivalia mavazi meupe ya kufanana ya jamii ya Wahindi, yanayojulikana kama sarees, huku picha nyingine ikimuonyesha Natasha akitengeneza vazi la nabii huyo huku wakitupiana tabasamu mwanana.

Wawili hao walikaribishwa katika Kanisa la Empowerment Christian lililoko Nairobi na mashemazi waliovalia mavazi vizuri ya kuvutia huku Carmel akiwa amebeba maua. Baadae walihubiri wakati wa ibada kwenye kanisa hilo.

MAISHA, ELIMU, UTAJIRI WA NABII NATASHA

Natasha ambaye anatoka katika familia ya kichungaji, Mama yake anayefahamika kwa jina la Esther Wanjiru pia ni Mchungaji kutoka Kanisa la Maximum Miracle Centre.

Natasha ambaye ana shahada ya Mawasiliano kwa Umma na Shahada ya Uzamili ya Theolojia anakadiriwa kuwa na utajiri wa Sh bilioni 2.4.

Licha ya kwamba hadi sasa haijawekwa wazi kuwa ni nani baba yake mzazi Natasha, hata hivyo inaelezwa kuwa Baba yake mzaliwa wa nchini Rwanda, wakati mama yake ndiye mwenye asili ya Kenya. Hata hivyo, amekuwa akinanusha mara nyingi kuwa yeye si Mnyarwanda.

Natasha ambaye ni mmoja wa watoto watatu katika familia yao, ni mmoja wa wachungaji wanaoishi maisha ya kifahari nchini Kenya baada ya mwaka 2019 kununua ndege yake binafsi, huku akiwa na magari kadhaa ya kifahari pamoja na majumba.

NABII STANLEY CARMEL

Nabii huyo aliyepewa jina la Nabii wa Kihindi, pia ni mtoto aliyetokea katika familia ya kichungaji.

Baba yake Carmel anayefahamika kwa jina la Saji Daniel ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la India Full Gospel Fellowship lililopo nchini India. Katika kanisa hilo ndiko Carmel alikopikwa na kisha kuamua kuweka makazi yake nchini Canada ambako ni mmoja wa wachungaji katika Kanisa la Markstreet United Church.

Nabii Carmel ambaye hajaweka wazi umri wake, naye anatajwa kuwa na utajiri wa Sh bilioni 2.3.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudika

NMB yawakutanisha Jay Meleody, Navy Kenzo Z’bar

Spread the loveMSANII wa kizazi kipya, Jay meleody akitumbuiza kwenye tamasha la...

Burudika

Man Mo; Mkali aliyetajwa na Hayati Magufuli mkutanoni

Spread the loveKILA mtu ana kipaji chake alichozaliwa nacho hapa duniani. Shida...

Burudika

Netta, Mr Eazi waangusha kolabo kali ‘Playground Politica’

Spread the loveMSANII maarufu wa muziki wa Pop, Netta amemshirikisha staa mkubwa...

Burudika

Kibao kipya cha Mr Eazi; Personal Baby

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr Eazi ameachia ngoma...

error: Content is protected !!