Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Nabi: ubingwa bado, subirini kidogo
HabariMichezo

Nabi: ubingwa bado, subirini kidogo

Spread the love

 

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mohammed Nasredine Nabi amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutulia kwa sasa kuhusu suala la ubingwa, kwani kwa sasa wanaangalia michezo iliyombele yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Nabi ameyasema hayo ikiwa ni siku moja toka klabu ya Simba iolipodondosha alama mbili kwa kulazimishwa sare na Azam Fc kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi.

Kabla ya mchezo huo tofauti kati ya wawili hao ilikuwa alama nane, na mara baada ya Simba kutoka sare hiyo kwa sasa tofauti ya pointi ni 10, kwa Yanga kuwa kileleni wakiwa na pointi 60 huku simba akiwa kwenye nafasi ya pili na pointi 50.

Akizungumza hii leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu suala la ubingwa, kocha huyo alisema kuwa kwa sasa suala l;a ubingwa bado kwani wanakabiliwa na michezo hapo mbeleni

“Yanga ubingwa bado, subiri kidogo, bado yanga hajawa bingwa mpaka itakapomuda wa kusema sasa hapa tayari hesabu ya ubingwa tutasherekea kwa muda huu bado tunaangalia mechi, ndani ya siku tisa tutakuwa na michezo mitatu.”

“Naumiza kichwa namna ya kupanga kikosi kwa hiyo mashabiki wasishangae kuona wengine wapo na wengine hawapo.” Alisema kocha huyo

Kwenye mbio hizo Yanga kwa sasa wanahitaji kushinda michezo mitatu kati ya saba iliyobaki sawa na pointi tisa, ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya 28.

Kwa kuzisaka alama hizo Yanga itashuka dimbani siku ya kesho kumenyana na klabu ya Mbeya kwanza, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku.

Mara baada ya mchezo huo Yanga itasafiri mpaka jijini Mwanza, ambapo itashuka dimbani kwenye mchezo ujoa dhidi ya Biashara United, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la CCM KIrumba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!