January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mzunguko Dodoma watengewa fedha

Makutano ya barabara za Dodoma mjini

Spread the love

JUMLA ya Sh. Milioni 165 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza sehemu ya mzunguko wa Shabiby kwenda makutano ya Chimwaga wilayani Dodoma. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Felista Bura (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua barabara ya mzunguko wa Shabiby hadi chako ni chako kwa nia ya kupunguza msongamano wa magari makubwa kuingia mjini itajengwa lini.

Akijibu swali hilo, Lwenge amesema  katika mwaka wa fedha 2015/16, jumla ya Sh. Milioni 165 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya mzunguko wa Shabiby kwenda makutano ya Chimwaga. 

Aidha, amesema  katika mwaka wa fedha 2014/15, jumla ya Sh. Milioni 360 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

Hata hivyo, amesema  ujenzi huo haukuanzia kipande cha Shabibiy hadi mzunguko wa uwanja wa Ndege kupitia chako ni chako kwa sababu ya ukosefu ea fedha za kufidia mali zitakazoguswa wakati wa ujenzi wa sehemu hiyo .

Amesema  kulingana na uthamini uliofanywa mwaka 2010 zinafikia jumla ya Sh. Bilioni 2.657.

error: Content is protected !!