March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mzungu kortini kwa kukutwa na fuvu la Nyumbu.

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

RAIA wa  Denmark Ricki Thomson (49), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  kwa kosa ka kukutwa fuvu la Nyumbu., Anaandika Faki Sosi.

Mtuhumiwa huyo amekutwa na fuvu hilo bila kibari cha Mkurugenzi wa wanyama pori nchini.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,  Cyprian Mkeha, Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa akiwa amedai  kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 9, mwaka huu katika Uwanja Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere bila kuwa na kibali.

“Ulikamatwa na fuvu hilo bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wanyama pori nchini,” amedai Kishenyi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mtuhumiwa amekana na upande wa Jamhuri umedai kukamilisha upelelezi
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 16, mwaka huu itakapokuja kutajwa.

error: Content is protected !!