Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mzimu wa Chadema waitafuna CCM uchaguzi wilaya
Habari za SiasaTangulizi

Mzimu wa Chadema waitafuna CCM uchaguzi wilaya

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM , Humphrey Polepole
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimezidi kuogopa kivuli cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kutimua wagombea wa uenyekiti wa wilaya ambazo Chadema kimeshinda ubunge, anaandika Hamisi Mguta.

CCM kimefuta majina ya wanachama waliopitishwa kugombea uenyekiti katika wilaya za Hai, Moshi mjini na Siha ambako Chadema kilishinda ubunge mwaka 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamprey Polepole ametangaza hayo leo, baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Polepole amesema wagombea wote waliofutwa wamebainika kuwa walikuwa na viashiria vya kuhatarisha uhai wa chama pamoja na kasoro mbalimbali.

Aidha, katika wilaya ya Musoma vijijini uchaguzi wa ngazi ya mwenyekiti wa wilaya pamoja na jumuiya zingine utafanyika baada ya chama kutangaza.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya CCM kuamua kupanua wigo na kugawa wilaya za Musoma mjini na Musoma vijijini.

Amesema kila mwanachama wa CCM anatakiwa muda wote kuzingatia maadili, kanuni na taratibu zote za chama na kwamba atakayekwenda kinyume chake atafukuzwa uanachama.

CCM kimetangaza kwamba hakuna mwanachama atakayeshikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja na kwamba hilo halina mjadala lazima mtu mmoja awe na kofia moja.

Polepole akizungumzia upande wa Zanzibar, amesema wamepata taarifa kuna watu wameanza kampeni kwa ajili ya kupata urais visiwani humo kabla ya wakati wake kufika na kwamba chama kimewaonya.

Kimewataka kuacha mara moja mpango huo vinginevyo wakibainika kwa ushahidi watatimuliwa ndani ya chama.

Kwa upande wa wanachama ambao hawakuridhika na maamuzi ya vikao kwa ngazi waliogombea wametakiwa kufkata rufaa ngazi ya juu yake ili kuhakikisha haki inapatikana.

Amesema kila mtu atapata haki yake kwa kufuata tataribu zilizowekwa na chama kupitia vikao. Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kikao hicho kimepitisha majina ya wenyeviti 161 wa wilaya za Tanzania Bara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!