
Waziri Mlkuu Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Sikukuu ya Idd ambayo kitaifa itafanyika Mkoani Geita kesho au keshokutwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la waislamu Tanzania Sheikh Suleiman Lolila Baraza hilo la Idd el Fitri amewataka waislamu wote nchini kuisherehekea sikukuu hiyo kwa kutoa zakatul fitri.
Aidha,amesema lengo la zakatulfitri ni kuwasaidia yatima , wajane na fukara, kuwatembelea wagojwa hospitali na kuwafariji kupitia sikukuu hiyo.
Sheikh Lolila amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni, kudumisha amani na utulivu hususani katika kipindi hiki taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu oktoba 25 mwaka huu.
Aidha, ametoa wito kwa wagombea wa nafasi mbalimbali kuacha kufanya kampeni chafu zitakazo hatarisha amani ya wananchi.
Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura li kutekeleza haki zao za msingi ya kupiga kura.
Kwa upande wa Jijini Dar es Salaam Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo.
Ibada hiyo itafanyika katika viwanja vya Mnanzi mmoja kuanzia majira ya saa moja na nusu asubuhi.
More Stories
TCRA yajitosha bei za vifurushi
Huawei yaunga mkono malengo endelevu UN
Watuhumiwa 5 ujambazi wauawa Dar, bastola…