December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mzee Moyo hatunaye

Mwanasiasa Mkongwe nchini na muasissi wa siasa za maridhiano Zanzibar, Nassor Hassan Moyo

Spread the love

VISIWA vya Zanzibar na Pemba vimepata pigo, Mzee Hassan Nassoro Moyo ambaye ni miongoni mwa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 18 Agosti 2020, mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya marehemu Moyo, mwili wa mwanasiasa huyo mkongwe utazikwa nyumbani kwake maeneo ya Fuoni visiwani Zanzibar, saa 10:00 jioni.

Enzi za uhai wake Hayati Moyo alikuwa miongoni mwa mawaziri wa katika Serikali ya Tanzania, ambapo aliwahi kuwa Waziri wa Sheria pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Akizungumzia kifo hicho, Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, Taifa limepaa pigo kwa kuondokewa na mwanamapinduzi visiwani Zanzibar.

Hayati Moyo aliongoza Kamati ya Maridhiano Zanzibar tarehe 5 Novemba 2009 iliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume na Maalim Seif Shariff Hamad katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisisasa visiwani humo, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Mwaka 2010.

Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa CCM, lakini alifukuzwa na Halmashauri Kuu yake ya Mkoa wa Magharibi mwaka 2015.

Zitto ameandika katika ukurasa wake wa Twitter akimuelezea Mzee Moyo kama mtu muhimu aliyefanikisha uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano visiwani humo.

“Kwa majonzi makubwa, nimepokea taarifa za msiba wa kuondokewa na M zee Moyo, mwasisi wa Mapinduzi, Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar. Mwenyezi Mungu ampe kauli thabiti na amlaze mahala pema peponi,” ameandika Zitto.

error: Content is protected !!