July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mzee miaka 61 akutwa na funguo 83 bandia, misumari 47 Dar

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

Spread the love

 

KAMANDA wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema, wanamshikilia Mzee Said Abdallah (61), baada ya kumkuta akiwa na funguo bandia 83, misumari ya aina mbalimbali 47 anazodaiwa kutumia kwa wizi. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Alhamisi, tarehe 6 Mei 2021, Mambosasa amesema, Mzee huyo, anatuhumiwa kwa wizi kwenye Maghala na maduka kwa kutumia funguo bandia.

Amesema, Mzee huyo Mkazi wa Mbagala Kilungule, alikamatwa tarehe 04 Mei 2021, huko Mbagala Kilungule akiwa na funguo bandia 83, misumari ya aina mbalimbali 47 ambayo ni malighafi za kutengenezea funguo bandia.

“Mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kufanya uhalifu tangu mwaka 2013 maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kutumia funguo bandia,” amesema Mambosasa

error: Content is protected !!