October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mzee Mangula ahimiza vikao kufanya maamuzi

Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapiduzi (CCM), Mzee Phillip Mangula, amesema vikao ni muhimu katika kutafuta makubaliano na kujenga umoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mzee Mangula ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 12 Oktoba 2021, akitoa mada ya mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kudumisha amani na umoja kwa maendeleo ya jamii, kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha muasisi huyo wa Taifa la Tanzania, lililofanyika jijini Dar es Salaam.

“Vikao vinajenga umoja kuhusu hayo mnayotaka kufanyia uamuzi, tofauti ya mawazo ndiyo kujadiliana,  kutoa mawazo yako mkubaliane kisha linakuwa lenu mnajenga umoja,” amesema Mzee Mangula.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema hata Mwalimu Nyerere alifanikiwa kujenga umoja kwa kufanya majadiliano  kwenye vikao.

” Mwalimu Nyerere alijenga umoja wa viongozi na usingeweza kupatikana huu umoja bila kukutana, alijenga mfumo msingi wa kukutana katika vikao ndani ya chama chake,  ana wazo lake analeta wanalikubali linakuwa wazo letu. Mmetofautiana katika mawazo kila mtu ameleta mawazo yake lakini mkiongozwa na viongozi wa kikao chenu mnafika muafaka mnakubaliana,” amesema Mzee Mangula.

error: Content is protected !!