Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mzee Makamba aibua mjadala majibu yake kuhusu mgawo wa maji, umeme
Habari za Siasa

Mzee Makamba aibua mjadala majibu yake kuhusu mgawo wa maji, umeme

Mzee Yusuph Makamba
Spread the love

 

KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuph Makamba, ameibua mjadala kufuatia kauli yake iliyowataka watu wanaohoji uhaba wa umeme na maji kuwa na shukrani kwa kuwa chama hicho hakiwezi kumaliza changamoto zote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mjadala huo umeibuka jan na Leo Alhamisi, tarehe 8 Desemba 2022, katika mitandao ya kijamii, baada ya Mzee Makamba kumshukia vikali mwandishi wa habari aliyemhoji Kwa nini anasema nchi Haina matatizo wakati Kuna uhaba wa maji na umeme.

Mzee Makamba alimshukis vikali mwandishi huyo, huku akimhoji anatakaje CCM imalize matatizo yote wakati yeye na baba yake wameshindwa kuyamaliza.

“We nyumbani kwako umemaliza yote? Baba Yako amemaliza yote? Mimi sijamaliza yote, unataka CCM Leo imalize. Ni Chama gani hicho? Kama haya huelewi, hutaelewa ya mtu mwingine,” alisema Mzee Makamba Jana akihojiwa na wanahabari jijini Dodoma

Aliongeza “we hukusoma?, Chuo kikuu umekijenga na baba Yako? Sisi miaka ya 60 tumeshindwa kusoma vyuo vikuu, Leo umekwenda chuo unasema nchi Ina matatizo.”

Kufuatia kauli hiyo, baadhi ya watu walitoa maoni Yao kupitia ukurasa wa Twitter.

Tonny Adamms, alikosoa kauli hiyo akisema siyo majibu ya busara “haya siyo majibu sahihi kwa mtu wa Rika lake, hasira za kushindwa ndiyo maana watanzania wanapigania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili pawepo na chaguzi huru zitakazowapumzisha wazee kama Hawa ambao wanahitaji kukaa pembeni baada ya kukaa madarakani Kwa kipindi kirefu mno.”

Mwanahatakati Fatma Karume, alichangia mjadala huo akiandika “kuweni na shukurani maana CCM Haina wajibu wa kuleta maisha Bora. Mmewapa madaraka ili watunishe misuli.”

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Chadema, John Heche alihoji “nani anawapa mawazo Hawa watu kufikiri kwamba nchi yetu ni Mali Yao na ni kama nyumba Yao.”

Regan Tesha aliandika “mzee wetu anasema vyuo hajajenga na baba yake, ni kweli ila pia vyuo havijajengwa na CCM. Vyuo vimejengwa na Kodi na majasho ya watanzania huku CCM akiwa kama mnufaika wa Kodi hizo Kwa kusimamia ujenzi Kwa malipo mazuri. Tusifanye Serikali inafanya mambo Kwa hisani jama.”

Naye Suleiman Al-Abriy, alihoji CCM inataka ishukuriwe Kwa jambo lipi wakati inaongoza takribani miaka 60, huku maji na umeme hakuna.

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania ilitangaza mgawo wa maji na umeme katika baadhi ya maeneo, ikisema kwamba changamoto hiyo inatokana na upungufu wa maji unaosababishwa na ukame ikiwa ni matokeo ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!