June 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwongozo mpya kuboresha taarifa za serikali  waandaliwa 

Spread the love

WAKALA ya Serikali Mtandao umeandaa mwongozo unaolenga kutoa utaratibu wa kufuatwa na kuzingatiwa katika kusimamia na kuendesha tovuti za serikali, anaandika Aisha Amran.

Muongozo huo pia utatumika kutatua changamoto  na kuziwezesha taasisi za umma kuandaa tovuti zenye mwonekano unaoshabihiana, utakaokidhi mahitaji ya wadau na pia kuwapa urahisi wa kutafuta taarifa au kupata huduma kupitia tovuti hizo.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo na Wakala ya Serikali Mtandao inaeleza mwongozo huo umeandaliwa kutokana na uwepo wa wa tovuti zisizokidhi viwango na ubora kufuatana na mahitaji ya watumiaji, gharama kubwa za uendeshaji, taarifa zilizopitwa na wakati, kutopatikana mara kwa mara.

Pia kukosa mifumo ya usalama ya kuzilinda na pia idadi kubwa ya tovuti hizo kuwa katika zama za kutoa taarifa tu na sio huduma.

Aidha, imebainisha changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili kuwa ni baadhi ya tovuti za taasisi za umma kutokuwa na taarifa mpya na za mara kwa mara, kutohusisha zilizopo na kutofuatwa mwongozo uliyowekwa na unaosisitiza usanifu wa tovuti hizo.

Taarifa hiyo imesema, katika kutatua changamoto hizo, maofisa mawasiliano na wataalamu wa TEHAMA wanaagizwa kuanza mara moja kuhuwahisha tovuti hizo na kuweka taarifa zao kwenye tovuti kuu ya Serikali na mwisho wa mwezi huu taasisi zitakazoshindwa kutekeleza zitaanikwa hadharani na hatua nyingine za kiutawala zitachukuliwa.

 

error: Content is protected !!