August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwizi wa kwenye mabasi jela mwaka mmoja

Spread the love

MWANAUME mmoja Kajuna Rweyemamu (32) mkazi wa Mbagala Majimatitu, Dar es Salaam amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumuibia abiria mwenzake Sh. 3 milioni, anaandika Christina Haule.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani wa Morogoro, Urlich Matei, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani baada ya kumkamata kufuatia kumnywesha juisi yenye madawa ya kulevya abiria mwenzake Novemba mosi mwaka huu, eneo la Kingululwira, Morogoro wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Kamanda huyo alimtaja abiria aliyenyweshwa aliyeibiwa ni Ibrahim Wiliam (38) mkazi wa Dodoma ambaye alipoteza fahamu na hatimaye kulazwa katika hospitali ya Rufaa Morogoro.

Amesema, mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo akiwa kwenye basi lenye namba za usajili T 669 DGB mali ya kampuni ya Shabiby Line wakitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Amesema kuwa mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakama ya mwanzo Kingululwira kwa kosa la wizi chini ya shauri la jinai namba cc.331/2016 mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Benadeta Mbawa na hatimaye Novemba 30 alihukumiwa adhabu hiyo.

error: Content is protected !!