January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwitikio wa Real Estate Tanzania ni mkubwa-Lukuvi

Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lema akimuelekza shughuli za Lamudi, Waziri wa Ardhi, Nyuma na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipotembelea banda hilo

Spread the love

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Watanzania wameanza kuelewa juu ya biashara ya mali zisizohamishika (Real Estate), huku akiwapongeza Kampuni ya Lamudi Tanzania kwa kuifanya biashara hiyo kwenye mtandao. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Lukuvi alitoa kauli hiyo alipotembelewa maonyesho ya biashara za nyumba yaliyopewa jina la Tanzania Home Expo yaliyofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza alipotembelea kwenye banda la Lamudi Tanzania, Lukuvi amesema, biashara ya Real Estate ilipoanza nchini ulikuwa inaonekana ni kitu cha ajabu, lakini siku zinazozidi kwenda ndipo inaposhika kasi.

Lukuvi ameipongeza Lamudi Tanzania kwa kurahisisha biashara hiyo kwa kuiweka mtandaoni, hivyo kuwapa urahisi Watanzania kuweza kununua nyumba, viwanja na mali nyingine zisizohamishika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick amesema kuwa miradi ya Real Estate imekuwa na msaada mkubwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na kupitia Lamudi wanaweza kufanikiwa zaidi.

Naye Meneja Mkuu wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa amesema biashara ya Real Estate inakuwa kwa kasi, lakini ina changamoto kubwa ya kuuzwa kwa fedha za kigeni badala ya shilingi ya Tanzania.

Meneja wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick kazi za kampuni hiyo, alipotembelea katika banda lao
Meneja wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick kazi za kampuni hiyo, alipotembelea katika banda lao

Nyagawa amesema asilimia kubwa ya biashara ya Real Estate inauzwa kwenye dola kitu ambacho kinamfanya Mtanzania kutoa fedha nyingi kulingana na thamani ya fedha, lakini ingekuwa kwa shilingi ingepunguza makali.

“Serikali inatakiwa kuangalia hili mara mbili, kwani mteja wa Real Estate atatumia fedha nyingi kununua eneo kutokana na biashara hiyo kuuzwa kwa dola,” amesema Nyagawa.

Maenyesho hayo ya siku nne, yamefunguliwa leo na yanatarajiwa kufungwa Jumanne ya Mei 5, 2015.

error: Content is protected !!