September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waitara ajikomba kwa Rais Magufuli

Mwita Waitara, aliyekuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira

Spread the love

MWITA Waitara, Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, jijini Dar es Salaam amejikomba kwa Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amemwambia Rais Magufuli kwamba, atavuna kura nyingi za urais kwa kuwa, nafasi aliyompa ya uwanaibu waziri wa TAMISEMI, umemuezesha kujua hilo kutokana na kutembea sehemu mbalimbali.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Januari 2020, katika hafla ya makabidhiano ya nyumba za maofisa na askari wa jeshi la magereza, zilizoko jimboni mwake (Ukonga), jijini Dar es Salaam.

“…mwaka huu utavunja rekodi ambayo haijawahi kupatikana kwenye taifa hili,” ameeleza Mwita na kwamba, alikopita uchaguzi wa rais umekwisha.

“Kote nilikopita wanasema, uchaguzi wa rais umeisha na utaweka historia, mara zote tukifanya uchaguzi huwa kura za urais awamu ya kwanza zinakuwa nyingi, inayofuata zinakuwa chache, naomba nikuhakikishie mwaka huu itakuwa vice versa (kinyume chake).” amesema Mwita.

Mwita amedai, Rais Magufuli atavunja historia katika matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, kwa kuwa uongozi wake umeacha alama kwa Watanzania wengi.

“Kwa nafasi uliyonipa ya naibu waziri, nimezunguka nchi hii, Bwana Yesu anasema, wasipoamini watu wake waamini kupitia matendo ya watu wake. Mhehsimwia rais Watanzania, wataamini kupitia matendo yako na ni kiongozi ambaye unaacha alama,” amesema Mwita.

error: Content is protected !!