July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwisho wa analojia Juni 17 – TCRA

Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy

Spread the love

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo 17 Juni mwaka huu, mikoa yote itatumia mfumo wa utangazaji wa televisheni wa digitali badala ya analojia. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungay, amesema mfumo wa matangazo wa digitali hadi sasa umeleta mafanikio makubwa nchini.

Amesema, miji ishirini inanufaika na matangazo yapatikanayo ya digitali, ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga, Moshi, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Singida, Tabora, Iringa, Songea, Musoma, Kahama, Sumbawanga, Bukoba, Mtwara na Lindi.

Mungy amesema faida ya digitali ni kuwa na matumizi bora ya masafa ya utangazaji, kupata huduma za ziada, vifaa vya kuhifadhia  kumbukumbu, havichukui nafasi kubwa na kuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu nyingi.

Ametaja faida nyingine kuwa ni kupata vipindi vya masafa marefu yaleyale, matumizi bora ya nishati, utunzaji wa mazingira na ubora wa picha na sauti.

Pia ametaja sababu za kusitisha kwa matangazo ya analojia, kwa muda uliowekwa kuwa ni  kutoa muda wa kutosha kwa nchi na wanachama kufanya tathmini ya kiufundi ili kuweza kurekebisha kasoro zote zilizojitokeza kufupisha kipindi  cha mpito chenye gharama kubwa.    

Amesema, “kati ya mitambo 59 ya analojia iliyokuwepo, 57 imezimwa.”

Mungy ameongeza kuwa TCRA inahsirikiana na Wizara Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na wadau wengine kutoa elimu kwa umma kuhusu kuhamia katika mfumo huo.

error: Content is protected !!