Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mwinyi ampa heko JPM, Mkapa na JK wamtaka asonge mbele
Habari za SiasaTangulizi

Mwinyi ampa heko JPM, Mkapa na JK wamtaka asonge mbele

Rais John Magufuli
Spread the love

MARAIS wastaafu wa Tanzania, wamepongeza Rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli, jinsi anavyoongoza nchi na kutimiza adhima ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Marais hao; Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wamesema hayo leo Jumamosi tarehe 30 Mei, 2020 wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Ikulu eneo la Chamwino jijini Dodoma.

Mwinyi aliyeongoza Tanzania kati ya mwaka 1985-1995 ameanza kwa kusema, yeye kitaaluma ni mwalimu, akipewa nafasi wanazungumza sana, “tunatoa pongeza maalum kwa Rais Magufuli, kwa njinsi anavyoiendesha nchi yetu kwa aina mpya mpya na nzuri nzuri. Ningependa kutoa shukurani zangu hadharani.”

Mwinyi amemshukuru kwa kuwakaribisha kwenye halfa hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi kwani amewakutanisha wote jambo ambalo huwa ni nadra.

Naye Mkapa aliyeongoza Taifa hilo kati ya mwaka 1995 hadi 2005, ameanza kwa kusema, “Mimi si msemaji, sikuwa mwalimu kama Mzee Mwinyi, nilikuwa mwandishi wa habari na kama mwandishi wa habari ni kuripoti kinachosemwa.”

“Shukrani kwa kukumbukwa na Rais Magufuli kwa kupewa zawadi ya ndege tuliowatunza kwa miaka 30  yangu, ya Mwinyi na Kikwete,” amesema.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Mkapa amesema, “Mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa, mazuri ambayo Rais wetu anayatekeleza kutimiza Ilani ya CCM na imani ya CCM. Tunakushukuru kwa uaminifu huo kwa chama na Serikali uliyoiunda.”

Amesema, katika uamuzi huo, ujenzi wa ofisi za Rais Ikulu Chamwino ni mgumu. “Sisi wote tulipokea uamuzi wa chama kuhamia Dodoma, Mwinyi alifanya, mimi niliendeleza jitihada hizo.”

Mkapa amesema, alipounda wizara ya Tamisemi yote ilikuwa Dodoma. Baraza la usalama wa Taifa lote lilikuwa linakutana Dodoma.

“Aliyenifuata (Kikwete) alitekeleza hilo kubwa zaidi kukamilisha ujenzi wa jengo la Bunge na Chuo Kikuu cha Dodoma,” amesema

Amesema, Rais Magufuli amefanya mengi yote na mabadiliko makubwa ya mji wa Dodoma na wizara zote kuhamia Dodoma na, “kubwa Ikulu kuhamia hapa na ndiyo maana nilipoambiwa kuhudhuria sikusita hata kidogo…mbele kwa mbele, endelea hivyo.”

Kwa upande wake, Kikwete aliyeongoza Tanzania kati ya mwaka 2005 hadi 2015 amesema, “Ndoto inatimia. Mwaka 1971 chama cha Tanu kiliamua makao makuu yahamie Dodoma na ni uamuzi ulifanywa ki demokrasia.”

Amesema, haukuwa uamuzi wa Mwalimu Nyerere pekee kwani ilipigwa kura kwa mikoa mbalimbali ambayo mingi ilikubali lakini Mkoa wa Pwani ulikataa.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

“Haukuwa uamuzi wa Baba wa taifa tu kwamba tunakwenda Dodoma hapana, mikoa ilishiriki na mkoa uliokataa ni wa kwetu sisi Pwani,” amesema

Amesema, uamuzi wa kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma haukuwa wa kidemokrasia kwani wapo waliotaka kijengwe Mwanza, Mtwara na maeneo mengine lakini hakukubaliana nao.

“Mimi nilivyokuwa Rais, nikasema nitajenga chuo kikuu kibwa kuliko vyote nchi cha kuchukua watu zaidi ya 40,000. Uamuzi huo haukuwa wa kidemokrasia bali niliufanya kama Rais,” amesema Rais Magufuli

Katika pongeza zake kwa Rais Magufuli, Kikwete amesema, “Naungana na wenzangu kukupongeza na tunaomba kazi hii ikamilike kama ilivyokusudiwa, kama rais alivyokusudia. Mungu akujaalie umri ili ushiriki katika kukata utepe wa kufunguliwa ofisi hizi.”

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Makongoro amemshukuruku kwa kuwakaribisha katika hafla hiyo ya uwekaji ujenzi  wa ofisi za Ikulu ambazo ni kubwa kama ambayo Kikwete alijenga Chuo Kikuu cha Dodoma.

Awali, Mkuu wa JKT, Brigedia Jenerali Charles Mbuge amesema, ujenzi wa jengo la ofisi ya Rais na utawala ulianza tarehe 12 Februari, 2020 na utakamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa. (ingawa hakusema ni lini).

Amesema ujenzi huo unafanywa na Suma JKT na mshauri ni Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) ambapo majengo hayo yanafanyika kwa umakini mkubwa kutokana na aina ya majengo yenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!