August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwinjilisti amvaa Magufuli, amuonya

Spread the love

KAMARA Kusupa, Mwinjilisti wa makanisa ya kipentekoste hapa nchini, amesema marurufuku ya mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya upinzani iliyotangazwa na Rais John Magufuli itavuruga amani ya nchi, anaandika Pendo Omary.

Kusupa ambaye ni miongoni mwa watu walioshiriki katika harakati za kuishinikiza serikali  kurejesha mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, amemuandikia barua Rais Magufuli yenye kichwa cha habari; “Msimamo wako utachochea maasi”.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kusupa amesema, kauli za Rais Magufuli ikiwemo ile kusema watakaoandamana ‘watakiona’ na kusema, ‘mimi sijaribiwi’ ni kauli zinazothibitsha namna rais huyo anavyokosa unyenyekevu wa kiuongozi.

“Ukiwa binadamu huna namna ya kuepuka majaribu, asiyejaribiwa ni Mungu pekee. Ndio maana hata mwokozi wetu Yesu alijaribiwa na pia alitufundisha kwamba tunaposali tumwombe Mungu atuepushe na majaribu.

Mheshimmiwa rais haki inayokuwezesha kuzunguka Manyoni, Singida, Nzega na Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha ukifanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi waliokuchagua, ni haki hiyo moja ndiyo waliyonayo Lowasa, Mbowe na wanasiasa wengine,” amesema.

Amemtaka Rais Magufuli, asiwaoneshe watanzania kwamba haki ya mwenyekiti wa CCM taifa inaanzia pale zilipoishia haki za wanasiasa wa vyama vingine kwani kufanya hivyo ni kuchochea maasi.

“Rais Magufuli anapaswa kuhakikisha, taifa halizalisahi wakimbizi kama yalivyotokea maafa ya tarehe 27 Januari, 2001 baada ya Chama Cha CUF kuandaa maandamano na Serikali kuyasambaratisha na kuchochea vurugu zilizozalisha wakimbizi, waliokimbilia nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,” amesema Kusupa.

 

error: Content is protected !!