Sunday , 2 April 2023
Habari za SiasaTangulizi

Mwingine apotea​

Mkurugenzi wa Idara ya Haki na Wajibu wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo
Spread the love

ADUL Nondo, mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye alikuwa mstari wa mbele kupinga kitendo cha jeshi la Polisi kumpiga risasi, Akwiline Akwelina, amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na Nondo zinasema, kabla ya “kupotea” hewani, mwanafunzi huyo alijitoa kwenye makundi yote ya mtandao wa Whatsapp aliyokuwa amejiunga.

Nondo ambaye ni mwenyekiti wa TSNP, amekuwa mstari wa mbele kushinikiza serikali kufanya uchunguzi wa mauaji ya Akwiline.

Akwiline aliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi la Polisi, tarehe 6 Februari mwaka huu, kwenye maeneo ya Mkwajuni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, akiwa ndani ya basi ya daladala.

Akwiline alikuwa akitokea maeneo ya Mabibo kwenda Bagamoyo kwa mafunzo ya vitendo.

Habari zinasema, taarifa rasmi kwa umma zitatolewa kwa waandishi wa habari saa majira ya 9:30 alasiri kwenye ukumbi wa Kituo cha Sheria na Haki Za Binadamu LHRC.

Katika siku za karibuni, kumeibuka kundi kubwa la vitendo vya utekaji, utesaji na mauaji nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!