January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwina Kaduguda ateuliwa kumrithi Nkwabi Simba

Mwina Kaduguda

Spread the love

BODI ya Wakurugenzi ya Simba, imemteua Mwina Kaduguda kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa klabu akichukua nafasi iliyoachwa na Swed Nkwabi aliyejiuzuru wakati wakisubiri mchakato wa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Uteuzi huo wa Kaduguda unakuja baada ya klabu hiyo kukaa kwa miezi miwili bila ya Mwenyekiti toka kujiuzulu kwa Nkwabi Septemba, 14 mwaka huu, huku taarifa ya klabu hiyo ikisema kuwa mchakato wa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo utatangazwa hivi karibuni.

Kaduguda anakwenda kumrithi Nkwabi ambaye alijiuzulu miezi 10 baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Novemba, 5, 2018 na kuwa mwakilishi wa wanachama katika bodi ya wakurugenzi baada ya kupitwa bila kupingwa.

Wakati huohuo, bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo imemteua Salum Abdallah kuwa makamu mwenyekiti wa bodi hiyo na uteuzi huo umeanza toka tarehe Novemba 19 mwaka huu.

error: Content is protected !!