Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Michezo Mwina Kaduguda aitaka tena Simba
Michezo

Mwina Kaduguda aitaka tena Simba

Spread the love

BAADA kukamilika kwa zoezi la uchukuaji fomu kuwania uongozi ndani ya klabu ya Simba, kamati ya uchaguzi ndani ya klabu hiyo imetoa orodha ya majina 21 ya wanachama waliojitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa bodi ya Ukurugenzi ndani ya klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Katika nafasi ya Mwenyekiti waliojitokeza ni watu wawili Swedi Khamisi na Mtemi Rmadhani, kwenye nafasi ya wajumbe kwa upande wa wanawake waliochukua fomu ni Jasmine Soudy na Asha Baraka, huku kwenye nafasi ya ujumbe waliojitokeza ni watu 17.

Waliochukua fomu za ujumbe ni Hussen Mlinga, Iddi Kajuna, Said Tuli, Zawadi Kadunda, Mohamed Wandi, Selemani Said, Abdalaah Mgomba, Christopher Mwansasu, Alfred Elia, Mwina Kaduguda, Juma Pinto, Ally Suru, Hamisi Mkoma, Abubakari Zebo, Omari Mazola, Patrick Rweyemamu na Seleman Seleman.

Kamati hiyo ya usajili pia imesema zoezi la urudishaji fomu litaanza siku ya Jumanne tarehe 11 septemba 2018 hadi Jumamosi 15 Septemba mwaka huu huku wakiambatanisha pamoja na nakala za vyeti vyao vilivyothibitishwa na vyuo husika.

Uchaguzi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu baada ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji ndani ya klabu hiyo na kwenda kwenye mfumo wa kibiashara ambao unaoenekana kuwa na manufaa makubwa kwa klabu kiujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

error: Content is protected !!