January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Waziri Kombani kuzikwa J’tatu Morogoro

Spread the love

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Ulanga Mashariki mkoani Morogoro, Celina Kombani unatarajiwa kuwasili leo alasiri ukitokea nchini India alikokuwa amelazwa kwa takribani mwezi mmoja akipatiwa Matibabu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Afisa Habari wa Bunge, Owen Mwandumbya amesema mwili wa Marehemu Celina Kombani utawasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na utapelekwa Hospitali ya Jeshi la Lugalo.

Wakizungumza kwa niaba ya familia, kaka wa marehemu Martin Ombeshi na mkwe wa marehemu Gerald Mlenge wamesema wameupokea msiba huo kwa masikitiko na kueleza kuwa maziko yatafanyika mkoani Morogoro siku ya Jumatatu, shambani kwake Lukobe na msiba utapelekwa nyumbani kwao Mahenge wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro.

error: Content is protected !!