Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwili wa Rais Angola waendelee kusota mochwari, mwanaye akata rufaa
Kimataifa

Mwili wa Rais Angola waendelee kusota mochwari, mwanaye akata rufaa

Jose dos Santos
Spread the love

 

BINTI wa Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Uhispania ulioamuru mjane wa marehemu apewe mwili huo kwa ajili ya kuandaa mazishi nyumbani kwake nchini Angola.

Kesi hiyo iliwasilishwa juzi tarehe 18 Agosti, 2022 na bintiye mwenye umri wa miaka 44, Tchize dos Santos. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Rais huyo wa zamani alitawala taifa hilo la Afrika lenye utajiri wa mafuta kwa mkono wa chuma kuanzia 1979 hadi 2017, alifariki mjini Barcelona tarehe 8 Julai, 2022 akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Tangu wakati huo, swali la lini na wapi atazikwa limeigombanisha serikali ya Angola na mjane wake, Ana Paula na baadhi ya watoto wake ambao sasa wakubwa.

Jumanne, wiki hii mahakama ya Barcelona iliamuru mjane wa marehemu Ana Paula apewe mwili wa mumewe kwa ajili ya maziko.

Hata hivyo, binti yake alikata rufaa, akisema mahakama haikuwa na mamlaka ya kutoa uamuzi kuhusu jambo ambalo kimsingi lilikuwa la madai, nyaraka za mahakama zilionyesha. Rufaa hiyo pia inadai kwamba dos Santos na Ana Paula walitengana tangu 2017 na hawakuishi katika hali ya kawaida ya ndoa.

Tchize dos Santos amesema mara kwa mara baba yake alitaka kuzikwa huko Barcelona ambako alikuwa akiishi zaidi tangu ajiuzulu mwaka 2017.

Pia amedai kuwa mazishi ya babake yakifanyika nchini Angola yataipendelea serikali ya sasa ya Joao Lourenco jambo ambalo linakwenda kinyume na matakwa ya baba yake.

Siku chache baada ya kifo chake, uchunguzi wa maiti ulifanyika kwa ombi lake kwa msingi kwamba alikufa katika mazingira ya kutia shaka.

Katikati ya Julai, mahakama ya Uhispania ilikataa kuachilia mwili wake hadi vipimo vikamilike na uchunguzi wa maiti ulionyesha alikufa kifo cha kawaida.

Wakati wa utawala wa dos Santos ambao ulidumu kwa takriban miaka 40, wanafamilia wake walitumia utajiri wa mafuta wa taifa hilo huku Waangola wengi wakisalia katika umaskini.

Alipojiuzulu mnamo 2017, dos Santos alimkabidhi Lourenco, waziri wa zamani wa ulinzi.

Lakini Lourenco alimgeukia na kuanzisha harakati za kupambana na ufisadi ili kurejesha mabilioni ambayo alishuku kuwa yalikuwa yamefujwa chini ya dos Santos, kampeni ambayo imelenga familia ya rais huyo wa zamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!