MWILI wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu (71), unazikwa leo Alhamisi tarehe 25 Februari 2021, katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Anaripoti Matrida Peter…(endelea)
Profesa Ndulu, aliyekuwa Gavana kati ya mwaka 2008-2018, alifikwa na mauti tarehe 22 Februari 2021, katika Hospitali ya Regency, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kuuga mwili wa aliyekuwa Gavanna wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu
Jana Jumatano, mwili wa Profesa Ndulu, aliyezaliwa tarehe 23 Januari 1950, ulilazwa nyumbani kwake, Mbweni, Dar es Salaam ambapo Ibada ya kumuombea na kumuaga, ilifanyika kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Profesa Ndulu, aliwahi kuwa Naibu Gavana kati ya mwaka 2007-2008 na baadaye kuteuliwa na Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania kuanzia 2008-2018
Leave a comment