Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwili wa Nditiye waagwa bungeni
Habari za Siasa

Mwili wa Nditiye waagwa bungeni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga marehemu Nditie
Spread the love

 

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Atashasta Nditiye (52), umeagwa bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Shughuli ya kuuaga mwili huo, imefanyika leo Jumamosi tarehe 13 Februari 2021, viwanja vya Bunge jijini Dodoma na kuhudhuliwa na wabunge, mawaziri na viongozi wa Bunge hilo, akiwemo Spika Job Ndugai.

Nditiye, aliyewahi kuwa naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, alifikwa na mauati jana Ijumaa saa 4 asubuhi, Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma alipokuwa amelazwa, baada ya kupata ajali ya gari jijini humo, tarehe 10 Februari 2021.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, familia ya marehemu pamoja na wabunge wote.

“Nimepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha Mhandisi Nditiye, kwa niaba ya Serikali, natoa pole kwa mke wa marehemu, familia na ndugu wote.”

“Mheshimiwa Nditiye amekuwa mtumishi wa Serikali kwa miaka mitatu kuanzia 2017 hadi 2020 na katika kipindi chake ndani ya Serikali, ametoa mchango mkubwa katika kusimamia sekta ya mawasiliano,” amesema Majaliwa

Amesema Mhandisi Nditiye aliweza kutumia uwezo wake wote kuhakikisha Serikali inapata mafanikio katika sekta aliyokuwa akiiongoza.

“Serikali tumempoteza mtu muhimu sana. Jukumu letu kubwa ni kumuenzi kwa kuendeleza mema yote aliyoyafanya katika kipindi cha uhai wake. Pia tuendelee kuombea kwa Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema,” amesema

Naye, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema msiba huo umewasikitisha sana kwani alikuwa mpole na alipenda kufanya kazi yake vizuri, hivyo amewaomba waombolezaji wote kila mmoja kwa imani yake amuombe mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Mhadisi Nditiye.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Suleiman Zedi amesema, kamati yao ambayo marehemu alikuwa mjumbe ilinufaika sana na uwepo kwa sababu alikuwa mtu mwepesi kufikika na hakuwa mchoyo wa maarifa.

Awali, akisoma wasifu wa marehemu, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kuandikwa alisema, Mhandisi Nditiye alizaliwa 17 Oktoba 1969 wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

Alisoma Shule ya Msingi Kabwigwa kuanzia mwaka 1975 hadi 1981 na baadaye alijiunga na Dar es Salaam Technical College ambako alisoma kuanzia mwaka 1984 hadi 1986 na kutunukiwa cheti cha uhandisi.

Mwaka 2008, alitunukiwa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano ya Simu katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na baadaye kuanzia mwaka 2011 hadi 2013 alitunukiwa Shahada ya Uzamili (MBA) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, Mhandisi Nditiye alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!