Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwili wa mwanafunzi aliyesombwa na maji wapatikana Salenda
Habari za Siasa

Mwili wa mwanafunzi aliyesombwa na maji wapatikana Salenda

Spread the love

MWILI wa mwanafunzi, Rashidi Makoye aliyesombwa na maji tare 17 Oktoba maeneo ya Makoka Unyamwezini, Kimara, Dar es Salaam umepatikana maeneo ya Salenda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Marehemu Rashid ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Makoka alisombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.

Pamoja na jitihada za kumtafuta mwanafunzi huyo ziliongozwa na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, wakazi na maeneo hayo na Jeshi la Polisi hayakuzaa matunda mpaka zilipofungwa.

Ifuatayo ni taarifa kamili iliyotolewa na Mbunge Kubenea, 

MWILI wa yule mwanafunzi aliyesombwa na maji, katika eneo la Makoka Unyamwezini, umeokototwa kwenye maeneo ya Salenda, jijini Dar es Salaam.

Rashid Charu Makoye, alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekonadari Makoka, iliyopo katika jimbo la Ubungo.  Alisombwa na maji, tarehe 17 Oktoba mwaka huu.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika bomba kubwa la Dawasco lililopo mpakani mwa Mtaa wa Kimara Baruti, kata ya Kimara na Makoka, kata ya Makuburi.

Mwili wa Rashid umepatikana Jumamosi iliyopita, tarehe 27 Oktoba mwaka huu na kwa sasa, umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Taarifa zinasema, familia ya mwanafunzi huyo imeweza kuutambua mwili wa ndugu yao huyo, kutokana na viatu alivyo kuwa amevaa kabla ya kukutwa na dhahama hiyo.

Nimeelezwa na mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makoka, Emmanuel Akyoo, kwamba kunahitajika takribani Sh. 90,000 (elfu tisini), kwa ajili ya kulipia gharama za kuhifadhi mwili katika hosipitali ya Muhimbili.

Aidha, mwenyekiti huyo wa mtaa amenieleza pia kwamba mazishi ya Rashid yamepangwa kufanyika kesho Jumanne, nyumbani kwao Mbezi, Makabe, ambako ndiko pia Rashd alikuwa akiishi.

Nichukue nafasi hii, kuwapa pole ndugu, familia, marafiki, walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makoka, kwa kumpoteza mpendwa wao – Rashid Makoye – kijana aliyekatishwa uhai wake, katikati ya matumaini.

Katika msiba huu, nitawakilishwa na Mheshimiwa Akyoo, kutokana na kuwapo kwangu bungeni, kunakoendelea kufanyika Mkutano wa Bunge.

Vile vile, napenda kuwahakikishia wananchi wa Makoka, Kata ya Makuburi na Kimara Baruti, Kata ya Kimara, kwamba mimi mbunge wao, ninaendelea na mipango yangu ya kujenga kivuko cha miguu katika eneo hilo.

Kwamba, pamoja na ghiriba, hila, matusi na kebehi, ikiwamo kunizuia kukutana na wananchi wangu, bado sijakatishwa tamaa. Ninaendelea kuwasemea, kuwatetea, kuwahudumia, pamoja na kuwaletea maendeleo.

Jambo ninalowaomba kwa sasa, kuzidi kuwa wavumilivu, wakati mimi mbunge wao, nikijitahidi kulimaliza tatizo la kivuko katika eneo lao.

Saed Kubenea (Mb),

Dodoma, 28 Oktoba 2019. 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the loveUSHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou...

error: Content is protected !!