October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Mugabe waibua vita mpya, familia yapata pigo

Spread the love

 

MWILI wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, aliyefariki dunia tarehe 6 Septemba, 2019 umeamriwa na mahakama nchini humo ufukuliwe na kuzikwa upya katika makaburi ya mashujaa wa nchi hiyo ambayo pia ni ya jadi. Anaripoti Gabriel Mushi (endelea…).

Hatua hiyo imekuja bada ya mahakama hiyo kutupa mbali rufaa ya watoto watatu wa Mugabe ambao ni Bona, Bellarmine na Tinotenda waliokuwa wanapinga hukumu ya mahakama ya kimila iliyoridhia mwili huo kufukuliwa.

Mei 2021 Mahahama hiyo ya kimila iliridhia shauri lililofunguliwa mahakamani hapo na Kiongozi wa Kimila ambaye ni Chifu wa Zvimba, Stanley Mhondoro aliyetaka mwili huo wa Mugabe ufukuliwa.

Chifu huyo alidai mwili huo ulizikwa kinyume na mila za kabila lao ambapo mbali na kumuagiza mjane wa marehemu, Grace Mugabe kutekeleza suala hilo pia alimuamuru kulipa ng’ombe kama fidia ya ukiukwaji huo wa taratibu.

Hata hivyo, baada ya watoto wa Mugabe kukata rufaa katika mahakama hiyo ya Zimbabwe, hukumu imebaki palepale kuwa mwili lazima ufukuliwe.

Katika uamuzi uliotolewa tarehe 10 Septemba 2021 na Hakimu wa Mahakama hiyo ya Zimbabwe, Ruth Moyo umeweka wazi kuwa watoto hao hawana haki ya kuzuia mwili huo kufukuliwa.

Aidha, watoto hao wamedai wanakwenda kukata rufaa tena katika mahakama kuu nchini humo.

Hadi uamuzi wa mahamaka unatolewa, mjane wa marehemu, Grace Mugabe hakuwepo nchini humo akidaiwa yupo nchini Singapore kwa matibabu.

Mugabe alifariki akiwa na umri wa miaka 95, alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 37 na kuzikwa kijijini kwake kwenye makazi yake kilomita 90 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Harare.

error: Content is protected !!