October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Mkapa watua salama Masasi

Spread the love

HELKOPTA iliyobeba mwili wa Hayati Rais mstaafu awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa imetua salama katika uwanja wa ndege mdogo wa Masasi mkoani Mtwara. Anaripoti Mwandishi W etu, Mtwara … (endelea).

Ndege hiyo imetua uwanjani hapo leo Jumanne tarehe 28 Julai 2020, saa 8: 50 mchana ikitoka Uwanaj wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mwili wa Mkapa utazikwa kesho Jumatano tarehe 29 Julai 2020 kijijini kwake, Lupaso Mkoa wa Mtwara alikozaliwa tarehe 12 Novemba 1938.

Viongozi mbalimbali wameupokea mwili huo wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Mara baada ya kuupokea, msafara wa kutoka uwanjani hapo kwenda kijijini, Lupaso unaendelea huku wananchi mbalimbali wakijitokeza barabarani kumuaga mpendwa wao.

Mkapa alifariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku katika moja ya hospitali jijini Dodoma kwa mshtuko wa moyo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!