May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa mbunge Khatibu kuzikwa Pemba leo

Marehemu Khatib Said Haji

Spread the love

 

MWILI wa mbunge wa Konde (ACT -Wazalendo), Khatib Said Haji (58), utazikwa leo Alhamisi, tarehe 20 Mei 2021, saa 10:00 jioni, Kisiwani Pemba, Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson, akisoma taarifa ya Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, bungeni jijini Dodoma, amesema, mbunge huyo amefikwa na mauti leo Alhamisi, saa 11:40 aljafajiri, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Dk. Tulia amesema, taratibu zinaendelea kufanyika ili kuwapata wabunge watakaowakilisha kwenye mazishi hayo huku akiahirisha shughuli za kikao cha Bunge kwa leo hadi kesho, kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Khatibu, hadi anafikwa na umati, alikuwa na miaka 58, baada ya kuzaliwa tarehe 31 Julai 1962.

Amekuwa mbunge kwa takribani miaka 10, kuanzia 2010-2020 akiwakilisha jimbo hilo kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) na katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020, Khatibu aligombea tena jimbo hilo kupitia ACT-Wazalendo na kuibuka mshindi.

error: Content is protected !!