May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Magufuli wasimamishwa ukweni kwake

Spread the love

 

MSAFARA wenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli, umesimamishwa nyumbani kwa mke wake, Janeth eneo la Sengerema mkoani Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Dk. Magufuli, alifunga ndoa takatifu katika Kanisa Katoliki la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Janeth mwaka 1989.

Janeth ambaye kitaaluma ni mwalimu, ni mzaliwa wa Sengerema mkoani Mwanza.

Msafara huo wenye mwili wa mme wake, Dk. Magufuli, umesimama kwa dakika takribani kumi ili waweze kumuaga mwana familia mwenzao, ambaye aliona eneo hilo la Busisi.

Msafara huo umevuka kwa kivuko eneo la Busisi ukichukua takribani dakika 30 kutoka Busisi hadi upande wa pili majira ya saa saba mchana.

Eneo hilo, kulikuwa na umati mkubwa wa waombolezaji, ulisimama ili waweze kumuaga ambapo ulichukua takribani dakika kumis aa 7:30 hadi saa 7:40 mchana, ambapo kulikuwa na umati mkubwa ukiwasubiri.

Pia, viongozi wa dini ya Kikristu na Kiislamu waliweza kupewa fursa ya kumwombea na kumuaga Dk. John Pombe Magufuli, aliyefariki akiwa na miaka 61.

Msafara huo, umesimama ukiwa unatokea Mwanza ambapo maelefu ya wakazi wa jiji hilo na maeneo jirani, wameuaga mwili wa Dk. Magufuli, aliyefikwa na mauti tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Mara baada ya kusimama ukweni hapo, safari ya kwenda Chato ikaendelea kupitia Sengerema- Geita- Katoro- Bwanga hadi Chato ambako kunatarajiwa kuwa na umati mkubwa ili kumuaga mpendwa wao.

error: Content is protected !!