Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya
HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the love

MWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia vitani nchini Ukraine akiipigania Urusi, Nemes Tarimo, umewasili nchini leo Ijumaa saa 10:25 alfajiri na kupokewa na ndugu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mwili huo ambao unadaiwa kuharibika vibaya kutokana na kukaa muda mrefu tangu marehemu afariki dunia tarehe 24 Oktoba 2022, umepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuongezewa dawa ya kuhifadhi.

Kutokana na hali hiyo ndugu wameeleza kuwa mwili huo utaagwa nyumbani kwake Saranga jijini Dar es Salaam ambapo pia itafanyika Ibada ya misa na baadae mchana utaanza kusafirishwa kwenda mkoani Mbeya kwaajili ya maziko.

“Mwili ulishuka uwanja wa ndege majira ya saa 10:25 alfajiri na sisi tulikuwa pale, tunaishukuru sana Serikali imetuunga mkono na ilitusaidia katika kuupokea na kuweka mambo yote sawa na baada ya kukamilisha taratibu zote za pale airport, tukaona tuupeleke Muhimbili kwaajili ya kuweka sawa zaidi ili watu waweze kuuaga,” amesema amesema Henry Sandu ambaye ni msemaji wa familia kuhusu utaratibu wa mazishi.

Waombolezaji wameendelea kufika nyumbani kwa Tarimo jijini Dar es Salaam na miongoni mwa waliofika msibani hapo ni makada wenzake akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ambaye alisaini kitabu cha rambirambi na kisha kuondoka na imeelezwa kuwa anaweza kurejea kuaga mwili wa Tarimo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!