May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Dk. Likwalile kuzikwa leo Mpiji Magoe

Dk. Servacius Likwelile

Spread the love

 

MWILI wa katibu mkuu wa zamani wa wizara ya fedha na mipango nchini Tanzania, Dk. Servacius Likwelile, unazikwa leo Jumanne tarehe 23 Februari 2021, Mpiji Magoe, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Likwalile, alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi, tarehe 20 Februari 2021, katika Hospitali ya Regency, jijini Dar es Salaam.

Ratiba ya mazishi ya mwili wa Dk. Likwalile, aliyewahi kuwa Mhadhiri wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ulilala nyumbani kwake, Mbweni.

Asubuhi ya leo, mwili wa Dk. Likwalile, utapelekwa Kigango cha Mtakatifu Yohane Mbatizaji Ndege Beach/Mbweni ambapo pia, kutafanyika shughuli ya kumwombea na kumuaga.

Baada ya shughuli ya kuaga kumalizika hapo, safari ya kwenda Mpiji Magoe, kwa maziko itaanza.

error: Content is protected !!