October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwijaku arudi uraiani

Burton Mwambe 'Mwijaku'

Spread the love

MSANII wa maigizo Burton Mwambe (35) maarufu kwa jina la Mwijaku, sasa amerejea uraiani baada ya kukaa siku tano mahabusu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mwijaku alipandishwa kzimbani kwa tuhuma za kusambaza picha za ngono kwenye mtandaoni, ambapo leo tarehe 3 Agosti 2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamucha kwa dhamana.

Awali, Mwijaku alipandishwa kizimbani tarehe 29 Julai 2020 na kusomewa shitaka la kusambaza picha za utupu kupitia mtandao wa Whatsapp.

Alisomewa shitaka hilo na Wakili wa Serikali, Mwanamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

Mtuhumiwa huyo alikana mashtaka hayo ambapo Hakimu Kabate alimpa mashrati ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. 500,000 kila mmoja.

Lakini pia wadhamini hao wote walitakiwa kuwa wasanii aidha wa filamu au muziki, wanaotambiliwa na Baraza la Sanaa (Basata) na kupewa baraka za baraza hilo.

Leo Mwijaku ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti alipewa na mahakama hiyo.

error: Content is protected !!