
Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji
TANZANIA ina jumla ya viwanda 49,243, ripoti ya sensa ya viwanda nchini iliyozinduliwa leo imeeleza hivyo, anaandika Pendo Omary.
Akizindua ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema viwanda hivyo vipo katika makundi manne kukingana na idadi ya ajira.
“Viwanda vidogo sana (mtu 1-4), viwanda vidogo (watu 5- 49), viwanda vya kati ( watu 50 – 99) na viwanda vikubwa kuanzia watu 100 na kuendelea.
“Kama tulivyoona taarifa yetu inaonesha Kuwait asilimia 85.13 ni viwanda vidogo sana, asilimia 14.02 ni viwanda vidogo, asilimia 0.35 ni viwanda vya kati na asilimia 0.5 ni viwanda vikubwa. Kupitia takwimu asilimia 99.15 ya viwanda vote nchini ni viwanda vidogo,” amesema Mwijage.
Mwijage ameitaja mikoa mitano inayoongoza kwa viwanda kuwa ni Dar es Salaam (7,444), Mara (3,549), Ruvuma (3,477), Morogoro (3,077) na Mbeya (2,864).
More Stories
Askofu Kilaini alaani Klabu ya Simba kutumia msalaba kwa dhihaka
NMB kunufaisha sekta ya kilimo Tanzania
Dk. Mwinyi: Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa