Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwijage: Bila ‘Tax Clearence’ hupati mchumba
Habari za Siasa

Mwijage: Bila ‘Tax Clearence’ hupati mchumba

Spread the love

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ametahadharisha kuwa, wasiokuwa na utamaduni wa kulipa kodi yanaweza kuwakuta aliyoyakuta kwenye nchi nyingine, ya kunyimwa mchumba. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Waziri Mwijage amesema hayo katika sherehe ya uzinduzi wa maonesho ya bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya mkoa wa Pwani, iliyofanyika leo tarehe 29 Oktoba 2018, wilayani Kibaha mkoani humo.

“Tunataka ifikapo mwisho wa mwezi watu kwa mapenzi yao waende kulipa kodi, yasije kuwakuta niliyo ona kwenye nchi fulani, unakwenda kuchumbia wanakuomba ‘tax clearence’, kama huna ‘tax clearence’ mchumba hupati,” amesema Waziri Mwijage.

Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage amesema serikali imedhamiria kujenga uchumi wa kitaifa ili ifikapo mwaka 2025 kipato cha mtanzania kiwe dola za Marekani 3,000 pamoja na kuwa na taifa la watu walioelimika na wepesi wa kujifunza.

“Tanzania tunajenga uchumi wa kitaifa sio uchumi wa taifa, ni uchumi wa kitaifa, ifikapo 2025 wastani wa kipato cha mtanzania katika huo uchumi wa kitaifa iwe dola 3000, kwa kila mtu kama milioni 7.5, lakini vile vile kufika 2025 tuwe na taifa la watu walioelimika na wepesi wa kujifunza,” amesema na kuongeza Waziri Mwijage.

“Tunataka katika huo uchumi wa kitaifa tuendelee kuwa na utulivu na mshikamano, tujenge taifa lenye utawala bora, ukizungumza utawala bora watu wanaiangilia serikali, hapana hata kutotii sheria ina maana na wewe huna utawala bora.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!