May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwigulu: Wamiliki wa nyumba msihamishie mzigo kwa wapangaji

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amewataka wamiliki nyumbaamewataka wasihamishie mzigo wa kodi ya majengo kwa wapangaji na badala yake wafike katika Ofisi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kuainisha idadi ya nyumba walizo nazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia amewataka wapangaji watakaolipishwa kodi hiyo  pindi watakaponunua umeme, wanaweza kuwasilisha malalamiko yao hata ofisini kwake ili yashughulikiwe.

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Septemba 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ufafanuzi wa tozo mbalimbali zilizoanzishwa Serikali hivi karibuni.

Amesema kodi kwa njia ya luku, si kodi mpya, ilikuwepo lakini kilichobadilishwa ni utaratibu wa ukusanyaji.

“Watu wanachanganya kuwa kila mwenye umeme atakatwa kodi, hapana… kwa sababu kuna mita milioni moja vijijini zenye matumizi madogo, zimeondolewa, vilevile baadhi ya wastaafu wamepata msamaha wa kodi hii,” amesema.

Amesema watalaam wanaendelea kufanya uchambuzi kwa kuwa kuna nyumba moja yenye mita zaidi ya moja jambo linalosababisha kulipiwa kodi zaidi badala ya kusomeka kuwa ni nyumba moja tu inayostahili kulipiwa kodi katika mita moja.

Aidha, amesema maboresho yatafanyika katika suala la usawa wa ulipaji kodi kwani haiwezekani mmiliki wa kiwanja kimoja chenye nyumba zaidi ya moja alipe kodi sawa na mmiliki mwenye nyumba moja kwenye kiwanja kimoja.

“Lazima kuwe na usawa, tunaendelea kuchambua hayo ili mtu mwenye kikubwa zaidi alipe zaidi, watanzania naomba mridhie hii ni kanuni ya kikodi.

“Unatakiwa kumtoza kikubwa zaidi aliye nacho ili umpe asiye nacho, kuna changamoto baadhi ya maeneo, ukiweka flat rate sio usawa,” amesema.

Kutokana na ujio wa kodi hiyo iliyoanza kutozwa Agosti 20 mwaka huu, TRA ilitoa ufafanuzi kuwa kila jengo la kawaida lililopo ndani ya kiwanja litalipiwa Sh12,000 badala ya Sh10,000 ya awali na Sh60,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50,000 ya mwanzo.

Kwa halmashauri za wilaya na miji midogo, nyumba za ghorofa zitatozwa Sh60,000.

“Kwa utaratibu huo mpya, kila mnunuzi wa umeme atakatwa Sh1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Sh5,000 kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wale wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hii kwa pamoja katika ankara ya mwezi,” alisema taarifa hiyo.

error: Content is protected !!