July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwigulu aleta tafrani Kagera

Mwigulu Nchemba

Spread the love

JINA la Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limeleta kizaazaa mkoani Kagera. Watu wasiofahamika wanapita kwenye makontena na maduka yaliyo kando ya barabara kuu ya Bukoba – Biharamulo na kuandika jina lake kuwa ndiye Rais 2015. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea)

Kutoka mkoani Kagera, MwanaHALISIOnline limedokezwa kuwa wananchi walioathiriwa na siasa hizo za urais kwa kuchafuliwa makontena na maduka yao ni waliyoko kado ya barabara maeneo ya Biharamulo, Muleba, Kemondo na Bukoba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, amethibitisha tukio hilo lakini akasema hajapata malalamiko rasmi kutoka kwa mwananchi yeyote hadi sasa.

Amesema “Ni kweli nimeona. Unajua huwa naenda sana maeneo ya Biharamulo na Muleba, sasa nimepita juzi nikaona hizo nyumba hata mawe zimeandikwa kwa rangi “Mwigulu 2015” ila sijaletewa malalamiko rasmi.”

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa mji mdogo wa Kemondo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakibanga, Cosmas Mutasingwa (Chadema) amesema “Nimepigiwa simu na wananchi wakilalamika kuchafuliwa kuta za majengo yao.”

Kwa mujibu wa Mutasingwa, baadhi ya wananchi wanadai kuwaona vijana hao wanaofanya kazi hiyo, kwamba wanatembea na gari aina ya Land cruiser ambapo huandika kwa rangi ya kupuliza na kasha kukimbia.

Amesema kuwa maandishi hayo yanasomeka “Mwigulu Nchemba Rais 2015 tunayemtarajia”. Kwamba wameanza doria ya kuwasaka watuhumiwa na kwamba wataripoti suala hilo polisi.

error: Content is protected !!