September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwigulu aanzia pagumu

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

MWIGULU Nchemba, Waziri wa Katiba na Sheria aliyeapishwa leo tarehe 3 Mei 2020, amepewa jukumu zito na Rais John Magufuli. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Waziri Nchemba anachukua nafasi ya Dk. Augustino Mahiga aliyefariki dunia siku juzi tarehe 1 Mei 2020 na kuzikwa jana tarehe 2 Mei 2020.

Waziri Nchemba ametumwa kuchokonoa chanzo kikuu cha ‘hofu’ kwa Watanzania, hasa kutokana na majibu wa Maabara Kuu ya Taifa kuyumba katika majibu ya vipimo vya maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Rais Magufuli akimwapisha Mwigulu Chato, Geita amesema, Maabara ya Taifa ina mashaka katika kutoa majibu ya vipimo vya virusi vya corona.

Amesema, upo uwezekano baadhi ya Watanzania waliambiwa wana maambukizi ya virusi vya corona wakati hawana, hivyo amemtaka Waziri Mwigulu kuchunguza na kubaini nini msingi wa matokeo yasiyoeleweka kutoka katika maabara hiyo.

Akizunguma namna alivyohakiki sintofahamu kutokana na maabara hiyo, Rais Magufuli na timu yake, walipeleka sampuli (ambazo si za watu) mbalimbali kwa ajili ya vipimo, lakini majibu yake yalimshangaza.

“Waziri nimekuapisha leo, itabidi mkafanye uchunguzi katika laboratory (Maabara) ya kitaifa ya Tanzania iliyokuwa inahusika kupima corona.

“Kuna contoversal (mkanganyiko) nyingi sana za ajabu, tuliona walikuwa wakitoa matokeo tu positive, positive, positive mara yingi.  Nilizungumza na vyombo vya ulinzi na usalama hapa na nikatoa maelekezo kwamba, embu nendeni mkacheki, hivi vipimo vikoje, vifaa vikoje,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kwamba, si kila kitu mnachopewa lazima kiwe kizuri. Wanaweza wakatumika watu, vinaweza vikatumika hivyo vifaa, lakini pia inaweza ikawa sabotage (hujuma) kwasababu tu hii ni vita.”

Kutokana na mkanganyiko huo, Rais Magufuli na tumu yake waliamua kupeleka sampuli zavitu, ndege, wanyama na oil ili kuthibitisha kama vipimo kwenye maambara hiyo vinafanywa sawasawa.

“Tulichukua sample (sampuli) za mbuzi, kondoo, papai, oili za gari na vitu vingine mbalimbali, tukavipeleka pale kwenye maabara bila ya wao kujua.

“Tukazipa majina sample ya oil kwa mfano iliyotoka katika gari tuliipa jina la Jabir Hamza mwenye miaka 30, ilileta negative (hakuna maambukizi).

“Tulipopeleka sample ya fenesi ambalo tulilipa jina la Sara Samweli miaka 45, matokeo yake yalikua inconclusive (haifahamiki) na tulipopeleka sample ya papai, tukalipa jina la Elizabeth Anne, miaka 26, papai lile lilikuwa positive (kuwa na virusi) kwamba lina corona. Maana yake maji mle ndani kwenye papai ni positive,” amesema.

Amesema, pia timu yake ilipeleka sampuli ya ndege aina ya Kware (tulipeleka sample ya ndege Kware, imekuwa positive (alikutwa na virusi).

“Tumechukua mbuzi akawa positive (alikutwa na virusi). Tukachukua kondoo akawa negative (hakuktwa navyo nakadhalika…,” amesema.

Kutokana na mazingira hayo, Rais Magufuli ameonesha mashaka kwa watendaji katika maabara hiyo kwamba huenda wanatumika ama wana ujuzi usiokidhi viwango.

“…maana yake mapapai yote yale yangewekewa isolation (yangetenwa). Ukipeleka fenesi, nayo yalikuwa yapelekwe isolation (yatengwe).

“Ukishagundua kitu hiki, lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanika katika vipimo hivi. Kwamba kuna mambo ya ajabu yanafanywa katika nchi hii, eidha wahusika wa laboratory (maabara) ile wamenunuliwa na mabeberu.

“…eidha hawana utaalamu whichi is not true (kitu ambacho si kweli) kwasababu maabara hii imetumika sana kwenye magonjwa mengine…”

Katika hali hiyo, Waziri Nchemba amepewa kazi ya kuchunguza kilichomo ndani ya maabara hiyo.
Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka Watanzania kutokuwa na hofu, lakini kuzingatia na kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha ugonjwa wa corona.

“Niwaombe Watanzania, hofu tuiondoe. Hili tatizo litaondoka na tuendelee kuchukua tahadhari ambazo zinatakiwa kuchukuliwa,” amesema.

error: Content is protected !!