July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwigullu “amvua nguo” Kikwete

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Spread the love

MWIGULU Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete amesema, ili serikali iweze kufufua viwanda vya nguo, maguni na samaki, ni sharti wananchi wafunge mikanda. Anaripoti Dany Tibason kutoka Dodoma … (endelea).

Aidha, Mwigullu ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara hadi wiki iliyopita amesema, kuna haja ya kubadilisha sheria ya kupambana na rushwa ili kila atakayepatikana na vitendo vya rushwa, afukuzwe kazi, afilisiwe pamoja na kufungwa jera kwa kosa la kuhujumu uchumi.

Kauli ya Mwigulu inatafsiriwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni ya kutoriodhishwa na hatua ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ambayo inadaiwa kuchukua hatua zisizokidhi katika kuwadhibiti watuhumiwa na ufisadi.

Akizungumzia wakati wa kutangaza nia yake ya kugombea urais, Mwigulu amesema, Watanzania wengi wanasumbuliwa na umasikini, ukosefu wa ajira na kwamba yeye ndiye suluhisho la matatizo hayo.

Alirejea wimbo uleule ambao umeimbwa na wanachama wengine wa CCM kuwa taifa linasumbuliwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umasikini wa kipato, ukosefu wa ajira pamoja na ukesefu wa huduma bora za kiafya.

Akizungumzia masuala ya rushwa alisema, kuna matatizo makubwa katika kupambana na rushwa na kujigamba ikiwa atafanikiwa kuingia madarakani, basi atamaliza tatizo hilo.

“Yeyote atakayebainika kupokea au kutoa rushwa mtu huyo atachukuliwa hatua zaidi na kufukuzwa kazi. Tutamfunga na kwamba kosa hilo litaangukia katika makosa ya uhujumu uchumi,” ameeleza.

Hata hivyo, Mwigullu ambaye ameingia serikali katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja, hakueleza wapi alikopata mabilioni ya shilingi anayodaiwa kuyatumia kukodisha vikundi vya hamasa na kampeni.

Mbali na hilo, Mwigullu amesema, wapo watu aliyodai wanaaminisha wananchi, kwamba “kuongoza nchi kunategemea uzoefu au kufanya kazi serikalini kwa muda mrefu.”

Alisema kuwa kuwa kijana au mzee pekee haina maana kuwa hiyo ndiyo sifa ya kuwa kiongzi.

“Inawezekana mtu akawa amefanya kazi kwa muda mrefu serikalini, lakini akawa wa kwanza katika kulitia taifa hasara,” ameeleza.

Alisema ifike hatua sasa siyo kila mtu aweze kulitumikia taifa kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.

Kuhusu mgawanyo wa rasilimali za taifa, mwanasiasa huyo ambaye amewahi kutuhumiwa kubambikizia wanasiasa wa upinzani kesi za ugaidi ametetea uchimbaji wa gesi asilia na kwamba hakuna makosa yaliyofanyika.

Alisema, “Kuna watu huko wanalazimisha kusaini mikataba na sasa hao nao walijue haiwezekani tukawa tunaletewa mafedha katika makaratasi na mengine yanaenda juu kwa juu hilo haliwezekani.”

Amesema ni aibu kuwa kila mwaka serikali inadaiwa Sh.100 bilioni  kwa ajili ya huduma za afya lakini cha ajabu ni kuwa fedha hizo hazipatikani na badala yake wananchi wanaambiwa wagonjwa wanunue dawa wenywe.

Kuhusu mikopo kwa wanafunzi, Mwigullu amesema, katika uongozi wake, hakuna sababu yoyote ya mwanafunzi mwenye sifa kukosa mkopo.

Alisema bado zipo familia nyingi ambazo zinakabiliwa na umasikini hivyo lazima kuna haja ya wanafunzi kupata mikopo.

Akizungumzia juu ya kufanya kazi kwa mazoea alisema kuwa wapo watendaji wengi ambao wanafanya kazi kwa mazoea.

Kuhusu Muungano

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano lazima itaakikisha inasimamia muungano wa Tanzania Bara na Zanziba sambamba na kuimarisha uchumi wao.

Alisema kuwa ni lazima kuimarisha bandari salama,viwanda bora pamoja na kuimalisha ulinzi na salama.

Akizungumzia masuala ya migogoro ya alisema kuwa ni lazima kuwa migogoro hiyo ikomeshwe na kuwepo mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi.

Alisema kuwa amejitathimini na kuhakikisha kuwa hatawavusha watanzania na kukomesha kufanya kwa mazoea,kusimamia rasilimali na kuzingatia usawa ndipo kufanya kazi kwa vitendo na wakati pekee ni sasa.

error: Content is protected !!