August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwezi Mtukufu watengua kanuni bungeni

Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetengua kanuni kanuni ya 153 (1) kutokana na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, anaandika Hamisi Mguta.

Hayo yameelezwa  bungeni leo na Jenister Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu.

Amesema, utenguzi huo umefanyika ili kuwezesha Bunge kuendelea na vikao vyake bila kuingiliwa na shughuli za kuabudu kwa wabunge ambao ni Waumini wa Dini ya Kiislam.

Kwa kawaida, bunge linajadiliwa hadi saa saba mchana na kuahiriswha hadi saa 10 jioni, huendelea kukaa hadi saa 2 usiku kisha huahirishwa hadi siku nyingine lakini sasa litaahirishwa kila siku saa 10 jioni mpaka mwezi utakapokwisha.

 

error: Content is protected !!