July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti wa wafanyabiashara aachiwa kwa dhamana

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa kutokana na mgomo wa wafanyabiashara

Spread the love

BAADA ya wabunge kuishinikiza Serikali iingilie katia sakata la mgomo wa wafanyabiashara wa maduka nchini, hatimaye Mwenyekiti wao, Johnson Minja ameachiwa leo kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Minja anakabiliwa na kesi ya kuchochea mgomo wa wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakifunga maduka yao mara kwa mara kupinga matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD’s) zinazoelekezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakidai zinawapunja.

Mgomo huo umeendelea kufukuta upya hivi karibuni katika baadhi ya mikoa baada ya kiongozi huyo kukamatwa tena na kufutiwa dhamana mapema mwezi huu akidaiwa kuhamasisha wenzake kufunga maduka kushinikiza TRA.

Hata hivyo, hatua hiyo iliwafanya baadhi ya wabunge kwa siku mbili tofauti wakiongozwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), kuhoji sababu ya serikali kumshikilia Minja badala ya kuketi na wafanyabiashara hao kumaliza mgogoro huo.

Mbinyi maarufu kama Sugu, aliungwa mkono na wabunge wa pande zote wakitaka Minja apewe dhamana kisha utafutwe ufumbuzi wa mgogoro huo ambao unawaathiri wananchi na kuikosesha serikali mapato.

error: Content is protected !!