February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti UVCCM arudishwa rumande

Spread the love

BAADA ya kukamatwa, Sadifa Khamis ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa leo amefikishwa mahakamani Dodoma kwa tuhuma za kugawa rushwa, anaandika Hamis Mguta.

Mwenyekiti huyo amerudishwa rumande mpaka Desemba 19 mwaka 2017 akituhumiwa kuwapa wajumbe soda na nauli.

Awali Sadifa pamoja na mjumbe mmoja wa UVCCM waliwekwa sero jana kwa tuhuma za kutoa na kupokeea rushwa kwa ajili ya kununua uongozi na leo .

Kitendo cha Sadifa kutuhumiwa, kimenukuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk John Magufuli kama ni jambo la aibu ambapo alisema kijana ambaye ana kashfa ya rushwa hasipatiwe nafasi yoyote ndani ya uongozi wa vijana kwa maana hawawezi kuwa watenda kazi wema ndani ya jumuiya hiyo.

Mbali na Rais Magufuli kukerwa na vitendo vya rushwa pia ametangaza kuifuta bodi ya UVCCM kwa maelezo kuwa haina msaada wowote kwa jumuiya hiyo.

error: Content is protected !!