Saturday , 3 June 2023
Home Kitengo Michezo Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo
Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the love

HEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu katika ligi ya Kimwanga CUP na mashindano ya Hawa Abdul Rede CUP yamepamba moto huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Shadrack Makangula, akiwataka vijana kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika mtanange huo kwa upande wa mpira wa miguu umezikutanisha timu za Ting Wayland ambapo ilifanikiwa kuvuka hatua ya fainali kwa kuchambana timu cha kituo cha kulea vipaji Lamasia FC kwa bao 2-0 huku upande wa Rede timu ya Kanuni ikifanikiwa nayo kwenda fainali kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manzese Princes.

Hayo ameyasema kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayopigwa katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, katika mashindano hayo ya kuwania ng’ombe aliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo, Bakari Kimwanga pamoja na Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Ubungo, Hawa Abdulraman ambaye amekutanisha mabinti nao kuwania ng’ombe katika michuano hiyo.

“Kwanza, nitumie nafasi hii kuwashukuru madiwani wetu kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuanzisha michuano ya mpira wa miguu na rede ambayo yote kwa ujumla wake yanawasaidia vijana wetu kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo, lakini pia inasaidia kupata exposure (fursa)  na kubwa zaidi kutengeneza mahusiano mazuri baina ya viongozi na wananchi.

“Hivyo ni vema kwa mashabiki, wakeleketwa na wananchi kwa ujumla ambao timu zao wanazozishabikia zimefuzu kucheza nusu fainali kuhakikisha kuwa wakati wa michezo hiyo inapoendelea wawe na utulivu wawapo uwanjani kwa sababu tutakapoanzisha vurugu uwanjani hapa tutawakatisha tamaa wadau, wahisani na viongozi katika kuanzisha ligi mbalimbali kwa ujumla wake,” amesema Makangula.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amewataka wananchi kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya aliwashukuru viongozi mbalimbali aliombatana nao na kuwaomba madiwani hao michezo hiyo iwe endelevu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

error: Content is protected !!