July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti TAHLISO kuburutwa kortini

Chuo Kikuu cha Dodoma

Spread the love

UONGOZI wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), unatarajia kumburutwa mhakamani Mwenyekiti wa Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Elimu ya Juu (TAHLISO), John Nzilanyingi. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Uongozi huo unamtuhumu mwenyekiti huyo ambaye alikuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Elimu UDOM kwa ubadhilifu wa kiasi cha Sh. 6.7 milioni sambamba na kughushi sahihi za ziongozi wa seriali hiyo wapatao 60 ili kujipatia fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari na kusoma maazimio ya Baraza la Mawaziri kwa pande zote mbili baada ya kujirudhisha na ushahidi na maelezo ya upande wa mtuhumiwa, Waziri Mkuu wa Shirikisho Chuo Kikuu cha Dodoma, Charles Josia amesema, uongozi kwa pamoja wamekubaliana kutoa azimio juu ya kiongozi huyo.

Josia alisoma maazimio hayo kuwa ni Rais Mstaafu wa John Nzilanyingi afikishwe mahakamani kwa kughushi sahihi za mawaziri, manaibu mawaziri na wabunge wa UDOCE na kudai suala hilo lifanyike mara.

Amesema, uongozi umekubaliana kutuma waraka kwa marais wa vyuo vyote Tanzania kupitia TAHLISO kuwajulisha juu ya ubadhirifu uliofanywa na Mwenyekiti wa TAHLISO.

Akisoma maazimio hayo Waziri Mkuu amesema, uongozi wa serikali ya wanafunzi umekubaliana Nzilanyingi arejeshe pesa zote ambayo alikiri kuiba kiasi cha Sh. Milioni 6.7 na akishindwa kufanya hivyo, azuiliwe kufanya mitihani yake ya mwisho.

Amesema, sheria za chuo zinatakiwa kuchukua hatua mara moja kwa kufuata Katiba ya UDOSO na kumsimamisha masomo mara moja ili kuweza kutoa fundisho kwa viongozi wengine.

Kiongozi huyo amesema, uongozi ulikubaliana wizara zote zilizobainika kufanya ubadhilifu wa pesa zirejeshe fedha hizo na kuzikabidhi kwa serikali mpya.

Nzilanyingi alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo amesema, hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa kuna taratibu za chuo ambazo zinaweza kuchukuliwa hatua.

Pia amesema, yeye hajahojiwa na serikali mpya ya wanafunzi na amaendelea na shughuli zake za mitihani huku akiwa Mwenyekiti wa TAHLISO.

“Mimi siwezi kusema jambo lolote, hapo chuoni kuna mkaguzi wa mahesabu ambaye anaweza kufanya kazi hiyo na kama atabaini kuwa, kuna ubadhilifu umefanyika basi sheria itafuata mkondo wake.

“Najua hao vijana wana mihemuko ya kisiasa na wanajaribu kufanya siasa jambo ambalo ni la kitoto.Mimi nimeishafanya siasa najua na hapa nipo nimetoka katika mitihani na najiandaa kurudi katika mitihani na pia ninafanya kazi ya TAHLISO,” amesema.

error: Content is protected !!