May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti Mpya Simba aanza na AS Vita, kutangulia DR Congo kesho

Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba

Spread the love

 

MWENYEKITI mpya wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ameanza kazi kwa kasi katika kuhakisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye michuano kimataifa kwa kutangulia nchini DR Congo, siku ya kesho kwa ajili ya kufanya maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya AS Vital. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba itashuka dimbani siku ya Ijumaa tarehe 12 Februari 2021, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa nchini DR Congo, ukiwa mchezo wa kundi A.

Akiongea na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu ili kujua ni kwa namna gani ataweza kukamilisha mchakato wa mabadiliko ndani ya siku 60 kama alivyoahidi kwenye kampeni zake na kusema kuwa “Huu ni mchakato wa sheria na tutatumia sheria kukamilisha kwa wakati.”

Mangungu aliendelea kusema kuwa kwa sasa anajiandaa na safari ya kwenda DR Congo, ambapo ataondoka siku ya kesho na huku mipango kuondoka kwa timu inafanyika na umma utapewa taarifa.

“Mimi naondoka DR Congo siku ya kesho ila timu bado inafanya taratibu nafikili hivi karibuni mtatangaziwa,” alisema mwenyekiti huyo.

Simba kwa sasa ipo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kwenye kundi A, sambamba na klabu za AS Vita, Al Ahly na El Merreikh ya Sudan.

Klabu hiyo itaanza kutupa karata yake ya kwanza siku ya Ijumaa dhidi ya AS Vita ugenini na mchezo wa pili utakuwa dhidi ya Al Ahly mabingwa watetezi wa kombe hilo utakaochezwa tarehe 23 Februari 2021, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!