November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti mpya Jumuiya ya Wazazi CCM atangaza mapambano Uchaguzi Mkuu 2025

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma

Spread the love

 

MWENYEKITI mpya wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhil Maganya, amesema ataiongoza jumuiya hiyo katika mapambano ya kusaka ushindi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Maganya ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Novemba 2022, muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo kwa kupata kura 578 kati ya 835, kwenye uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika mapema leo Ijumaa.

“Tumemaliza uchaguzi wetu wa jumuiya lakini 2024 tuna uchaguzi, mimi nimeshapewa mamlaka sasa naaza kuelekeza kazi. Sisi jumuiya wazazi tunatakiwa tuwe mbele kuhakikisha kwamba tunaongoza jitihada za kushinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025, sisi lazima tuongoze mapambano haya,” amesema Maganya.

Aidha, Maganya amesema atamuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuupiga mwingi.

“Ninamwambia mama kwamba atapata ushirikiano, nitampa sapoti na huo upigaji mwingi ataendelea kupiga. Anayetaka kufa na afe mama ataendelea kupiga mwingi, nitamsapoti nitampa kila msaada na kila aina ya ushirikiano,” amesema Maganya.

Akielezea vipaumbele vyake atakavyotekeleza katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano, Maganya amesema atahakikisha jumuiya hiyo inakuwa na hospitali yake ya rufaa, benki pamoja na mashamba kwa ajili ya uzalishaji mali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake, Dk. Edmund Mdolwa, amewataka wajumbe wa jumuiya hiyo kuwaunga mkono viongozi wapya waliochaguliwa kwa nguvu zao zote.

Dk. Mndolwa ameshindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa leo, baada ya kupata kura 16 kati ya 835.

error: Content is protected !!